Wapenzi wa Madera mapya wakati wa msimu wa Ramadan

Posted on

Wapenzi wa madera mapya wakati wa msimu wa Ramadan

Kama ulikua hujui, wapenzi wa madera wapo sana wakati wa Ramadhan. Ramadhan hua ni msimu muzuri sana wakuongeza mapenzi kwa wanaopendana. Watu hua katika harakati zakuombea dua zao na kwahilo mapenzi huchangia pakubwa maana kitu upendo (love), mwenyezi Mungu hulifurahia.

Lakini mbona wanawake watamani sana kununuliwa madera wakati wa ramadhan?
Sikuzote hua tunatambua kua zawadi yoyote hua ni kitu kizuri sana kwa mwenye anae zawadiwa. Roho huu jawa na furaha na kwahilo baraka humrudia mwenye alietoa zawadi; kwahilo utakapo ombwa zawadi mfano wa dera, tena kwa msimu wa ramadhan, ni wakati kufahamu baraka utakazo zipata kutoka kwa Mola manake hakuna zawadi huenda burebure tu.

Nani wakupewa zawadi
Kwa maisha ya mtu yoyote yule tunafundishwa kwamba wanaozini hukosa baraka, kwahilo nibora sana kabla hujatoa zawadi yako, ukue macho kwa unaye taka kumzawadia manake unaweza kumpea mtu kitu kama zawadi lakini badae kitu hicho kikaja kukuletea shida nyingi mfano mikasa ya ajabu ambayo hujawai ona maishani. Sio kila binadamu unae mwona akiswali ni mtakatifu, wengine wakirudi manyumbani mwao wana mambo yao hufanya ambayo hayawezi karibiana na Mola, mtu kama huyo kaa mbali sana na yeye manake maisha yanasongea kila siku na haitokua kitu kizuri ukisongea pamoja na matatizo.