Safari Yangu
Nilikuja Nairobi kufanya kazi ya nyumba. Iyo ndio kazi ambayo nilikua nikifanya, tumeifanya for long mpaka 2019 ndio nikapata nafasi yakuenda middle east, Saudia. Maisha haikua vile nilivokua natarajia kabisa, maisha ilibadilika. Tuseme ukiingia, hujui iyo lugha, bado unafundishwa kazi, kupika ivo ndio vitu nilikua nafundishwa. After ukishajua pia, unaona kazi inakua ngumu. Sikama vile unaezakua umezoea. Ukifika huko sasa ndio unajua ugumu yenyewe si rahisi. Changamoto ya kwanza niliyopata ilikua ni kutolala. Kutopumzika. Kazi ilikua ni nyingi, nilikua nikilala saa kumi. Kulala kwangu nakuamka ilikua inategemea sazingine vile nitamaliza kazi. Unapata sazingine unamaliza kazi saa tisa ama saa kumi, sa wadosi wakilala ndio unapata mda pia wakulala.
Nalafu changamoto ingine ambayo ilinisukuma kabisa nikatamani niwe nirudi nyumbani uyo mzee sikumoja alipeleka bibi yake salon, na akarudi tu kama kawaida, sasa akaniambia nimtengenezee chai, nikaenda jikoni kutengeza chai, nilivofika jikoni nikamwona nae amenifwata, dakika kidogo nikasikia ameanza kunishika. Hapo tukaanza kumenyana lakini alinishinda nguvu, lakini hakunifanyia kitu bahati nzuri simu ikalia, akaniacha nikakimbia kulia kama 30 mins.
Immediately iyo kitu ilivo happen nilipigia agent kwasababu huezi enda kwa polisi direct. Hujui kama watakwamini ama hawatakwamini. Time yakurudi nyumbani kitu nilifanya vibaya, sikuwai jua kama ma agents walikua wanangojea pesa ya mashahara wangu nusu. So tym yakurudi walikua wamekasirika. Ma nguo walinipokonya, nalafu wakanipea karatasi ni sign kua wamenilipa pesa zangu zote na walikua wamechukua nusu na wakanipea nusu ya ile saving yangu yote nilikua nikisave.
Donate to Helen 0707901246